Maombi ya mlimani ni maombi yenye
kusudi maalumu yanayofanyika mlimani, porini,shambani, chumbani, pembeni mwa
bahari,mto ziwa au eneo lolote ambalo kuna utulivu wa kutosha.[1]
.
Nyakati zote za safari ya kanisa tangu Edeni, kanisa limepitia katika uzoefu
wa maombi ya mlimani. Uzoefu huu wa maombi ya mlimani unathihirika wazi wazi
katika kitabu cha Matendo.
Maombi ya mlimani ilikuwa ni moja ya kanuni
aliyoitumia Mtume Paulo katika kuotesha na kuliongoza kanisa katika kipindi
kigumu cha kanisa la mitume.
Lyrene akiandika katika kitabu chake cha “Prayer
and Evangelism” anasema kuwa “Kanuni ya
Maombi ya pamoja, au maombi ya kusudi na nia moja, ni mkanda unaofunga kitabu
kizima cha Matendo ya Mitume. Maelezo ya awali ya
Daktari Luka kuhusu wale 120 (Mdo.1:15) yanaonyesha
kufuatwa na agizo la Kristo la kumsubiri Roho Mtakatifu kwa kutii na kuomba kwa
nia moja kama kundi. Nguvu ya maombi ya pamoja inatambuliwa tena wakati Baraza
la Sanhedrin walipotishia wafuasi wa Yesu kwa kuwakataza na kuwatisha kuwa
wataadhibiwa kama wataendelea kuongea kuhusu “jina la Yesu”(Mdo.4:18). Nia ya
kuhubiri ilikuwa kubwa sana, hata hivyo, na mikutano ya maombi ya pamoja
ilielekezwa kwa kanisa la awali kama daraja jipya la ujasiri (Mdo.4:31).
“Wakiwa na ujasiri katika kushuhudia, walikuwa wote ni majasiri katika maombi."[2] Kama maombi haya
yalivyohitajika kwa kanisa la awali; kwa sasa bado ni hitaji kubwa kwa kanisa
la karne ya 21.
Zifuatazo ni mbinu 10 za kusaidia kuomba maombi ya mlimani
1. Chagua Muda mzuri (Mhubiri 3:17)
2. Chagua mahali pazuri penye utulivu (Marko 1: 35)
3. Ikiwezekana siku hiyo iweni katika kufunga ( Mathayo 6:6-18)
4. Shirikisha rafiki zako (Mhubiri 4:9-10)
5. Tumia mikao inayokupa uhuru na isiyochosha wakati wa maombi
6. Kuwepo na muda wa sifa, shukrani na shuhuda za imani (Zaburi 50:15)
7. Ikiwezekana tumia muziki uliotulia wa kumwabudu na kumsifu Mungu (2Nyakati 5:12-14)
8. Epuka kuvunja taratibu za kidini na kijamii. (Warumi13:1)
9. Kuwepo na Muda wa kusoma na kulitafakari neno la Mungu kwa wingi.
10. Kuwepo na ratiba maalum ya tukio na ifuatwe.
- Jina la kipindi na mhusika wa kipindi
- Muda wa kipindi
- Mambo ya kuombea
- Muda wa mapumziko, kutafari binafsi
[1] Igin
Soka, Kwanini Maombi ya Mlimani, Masomo ya maombi ya Wainjilisti walei -TPC
Effort, 1997
[2] Notable exceptions to this statement must be
recognized. For a concise summary of the issue see E. C. Lyrene, Jr.,
"Prayer and Evangelism," Evangelism in the Twenty First Century (ed.
by T. S. Rainer; Wheaton: Harold Shaw, 1989), 99.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni