Zifuatazo ni tofauti Saba kati ya Mfanyabiashara na Mjasiriamali
Mfanyabishara anaogopa mabadiliko wakati
Mjasiriamali anafurahia Mabadiliko
Mfanyabishara hana dira wala mwelekeo
wa biashara yake lakini
Mjasiriamali anao mwelekeo wa bishara yake.
Mfanyabiashara hajitumi na hugusa hiki na kile
bila kukikamilisha
wakati Mjasiriamali hujituma na kutumia nguvu na mali katika jambo moja
.
Mfanyabiashara si mbunifu na ni tegemezi; anaiga
wengine lakini
Mjasiriamali ni mbunifu na mwenye kujitegemea .
Mfanyabiashara
anafanya kazi zake kwa mashaka hana
uhakika na maisha ya baadaye ila Mjasiriamali
anafanya kazi kwa matumaini ya siku za baadaye.
Mfanyabiasha ni Mwoga
kufanya maamuzi wakati Mjasiriamali
haogopi kufanya maamuzi.
Mfanyabiashara
hana akili ya kujifunza; yeye
anapendelea kuiga wengine na hana mtandao wa biashara wakati Mjasiriamali anayo akili ya kujifunza
na anao mtandao wa biashara.
(Chiraka Muhura, Ujasiriamali Kwa
Maisha Bora,(Dar-es-Salaam :Hope
Publishers, 2014) 22)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni