Kitabu cha Danieli
Sura ya Tisa kinatoa mfano elekezi wa Maombezi . Katika Ombi hili
la Danieli tunapata sifa za mwombaji au sifa za ombi lenyewe kama ifuatavyo.
i. Mwombaji anakubaliane na Neno la Mungu
“Katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli kwa kuvisoma
vitabu nilifahamu hesabu ya miaka ambayo
neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii . .
. .” (Daniel 9:2)
ii.
Mwombaji aonyeshe uzalendo
“Nikamwelekezea
Bwana Mungu uso wangu ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga na kuvaa nguo za magunia na majivu”(Daniel 9:3)
iii.
Mwombaji ajikane nafsi
“Nikamwomba
Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mwenye kutisha
ashikaye maagano na rehema kwao wampendao na kuzishika amri zake” (Daniel 9:4)
iv. Mwombaji asijitenge na watu wa
Mungu
“Tumefanya
dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha
maagizo yako na hukumu zako.” (Danieli 9: 5)
v.
Mwombaji aimarishwe na
Toba
“Tumefanya
dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha
maagizo yako na hukumu zako . . . wala hatukusikiliza watumishi wako,manabii
ambao kwa jina lako walisema na Wafalme wetu . . . Ee Bwana haki ina wewe,
lakini kwetu sisi kuna haya ya uso kama hivi leo . . . Rehema na msamaha ni kwa
Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi. . . Na sasa , Ee Bwana Mungu wetu
uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari, ukajipatia
sifa, kama, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu “(Danieli 9: 5-15)
vi.
Mwombaji aitegemee tabia ya Mungu
“Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama,
nikasema, Ee Bwana, Mungu mwenye kutisha ashikaye maagano na rehema kwao
wampendao na kuzishika amri zake. Ee Bwana haki ina wewe lakini kwetu sisi kuna haya ya uso . . .
Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu ingawa tumemwasi. Na sasa , Ee Bwana
Mungu wetu uliyewatoa watu wako hawa katika nchi ya Misri kwa mkono hodari,
ukajipatia sifa, kama, kama ilivyo leo; tumefanya dhambi, tumetenda maovu “(Danieli
9:4, 7, 9, 15)
vii.
Mwombaji awe na lengo
la kumpatia Mungu utukufu
“Ee
Bwana sawasawa na haki yako yote nakusihi hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe
na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima
wako mtakatifu, maana kwa sababu ya dhambi zetu na maovu yetu ya baba zetu . . . Ee Mungu wangu tega sikio lako ukasikie
fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji uke ulioitwa kwa jina lako;
maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya
rehema zako nyingi. . . Ee Bwana, usamehe;
Ee Bwana,usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe Ee Mungu wangu; kwa
sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.”
(Danieli 9:16-19)
Kwa kujifunza zaidi jipatie kitabu kiitwacho "MAOMBI NA MAOMBEZI" Wasiliana na 0788010398.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni