Matumizi mabaya ya raslimali za mwajiri bila ruhusa kutoka kwake kufanya hivyo; hali hii inaitwa kitaalamu ni wizi kazini. Kwa kifupi inaitwa ni wizi wa wafanyakazi.
Zifuatazo ni aina sita za wizi katika maeneo ya kazi.
1.Wizi wa Muda. Kutokutunza muda wa kuingia kazini na kutoka kazini.Kujipatia likizo bila idhini ya mwajiri.
2.Wizi wa taarifa za biashara. Mfanyakazi anapotoa siri za biashara nje bila idhini ya mwajiri wake.
3. Wizi wa fedha taslimu. Wizi huu umekithiri sana kwani wafanyakazi wengi wamekuwa wakijichukulia fedha za waajiri bila ridhaa ya waajiri wao. Wengi wamefanya kwa kutumia utaalamu wa kuwaficha sana waajiri wao na wengine wamefanya waziwazi na kuyakimbia maeneo ya kazi.
4. Wizi wa matumizi ya ofisi. Wizi huu umekidhiri sana katika maeneo mengi haswa pale ambapo waajiri wanapokuwa makini katika ufuatiliaji wa mambo ya fedha. Ununuzi ya vitu vya ofisini unafanyika kwa maridhiano na muuzaji kuongeza bei na kutoa risiti. Wizi kama huu ni vigumu kuutambua ila kwa baadaye hawa wawili wakikosana siri hii itajulikana.
5. Wizi wa bidhaa au huduma zitolewazo na Mwajiri. Kuna uwezekano mkubwa wa mwajiri kuibiwa bidhaa au huduma. Wafanyakazi ambao siyo waaminifu wamekuwa wanachukua bidhaa za ziada kwa kukubaliana na mtunza stoo kuzidishiwa ili wagawane kipato baadaye.Huu ni wizi.
6. Kuwazidishia wateja bei ya huduma au bidhaa. Mfanyakazi anaweza kuongeza bei ya bidhaa kwa mteja na ongezeko hilo akaweka mfukoni. Ni vigumu kumpata mwizi kama huyu ila wewe mwajiri utamtambua kwa kusikiliza manunguniko ya wateja wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni