SOKA IGIN

WE INSPIRE AND EMPOWER FOR CHRIST'S MISSION.

Ijumaa, 23 Machi 2018

WATOTO WA BABA MMOJA WASIOFAHAMIANA



Nabii Ibrahim ambaye ni rafiki wa Mwenyezi Mungu anasimama kama baba yetu wa Imani zote na ndiyo maana jamii ya Wakristo na Waislamu wanayo asili moja ambayo ndiyo iwafanyayo wasimame imara hata leo.
Lakini twaweza kujiuliza swali  ieweje mimi mwislamu  niwe na asili moja na mkristo kupitia kwa  Ibrahimu na tusifahamiane? Huo undugu ulianza lini?;ndiyo maana hata Miriam (dada yake Musa) alipata ukoma kwa kumsimanga Sipora(Mke waMusa) alipomhoji kaka yake kuwa umemwoa mwanamke mweusi sana tena ambaye siyo uzao wa Ibrahim! Asijue kuwa naye Sipora alikuwa uzao wa Ibrahimu Kupitia kwa mkewe wa tatu aliyeitwa Ketura (Mwafrika mweusi kutoka Ethiopia)hivyo kwa hilo tu Mwenyezi Mungu akakasirika akampiga kwa ukoma(Hesabu 12:1-9);Na hili linajirudia katika karne yetu je wakristo na waislamu ni wote ni wa Uzao wa Ibrahimu?

       Sasa ni kwa vipi tunakuwa uzao wa Ibrahimu? Undugu kati ya Mwislamu na Mkristo umetokea mbali;
  •  Namna ya kwanza  inahusu uzazi wa kimwili ambao ni wale wote waliozaliwa na Ibrahim kupitia kwa Hajiri ambao ni uzao wa Ishmaeli 
  • Namna ya pili niWaliozaliwa na Ibrahim kupitia kwa mkewe Sara ambao ni uzazi wa Isaka
  • Mwisho ni Uzazi wa Imani ambao ni kwa wote wanaomwamini Masih Isa(Yesu);wote hawa wanahesabiwa kuwa wana wa Ibrahimu (Wagalatia3:29)
  •      Hata hivyo ndugu msomaji ni vizuri utambue kuwa Ibrahim hakuishia kwa mke wa pili bali katika uzee wake alimwoa mwanamke mwingine Mwarabu Mweusi(Mkushi) kutoka Ethiopia ambaye anamzaa Midiani na huyo Midiani anamzaa Yethro na Yethro anamzaa Sipora mke wa Musa.ambaye historia inasema yeye ni  asili ya kabila nyingi za Waarabu (Mwa.25:1-6;1Nyak.1:32;Kut.18:10-11) American Tract Society Dictionary).
Nipende kukujulisha kuwa changamoto kubwa ya kufahamiana ipo katika uzazi huu wa imani na ndiyo maana  Masih Isa katika kitabu cha Injili anasema kuwa uzazi huu wa sisi kuwa wana wa Ibrahimu kwa imani si uzazi wa damu wala mapenzi ya mwili wala mapenzi ya mtu bali kwa Mungu yaani kwa lugha nyingine wote wanaomwamini Masih Isa(Yesu);wote hawa wanahesabiwa kuwa wana wa Ibrahimu (Yonana1:13)

Inatia moyo sana kwani koo hizi mbili upande wa Ishmael (Waislam) na Ishaqa(Wakristo) tangu enzi za Nabii Ibrahimu wamekuwa na Umoja thabiti katika matukio Muhimu ambayo hata kwa sasa twaweza kuendeleza katika wakati wetu ili kuwaenzi wazee wetu na kumpatia mwenyezi Mungu utukufu.
  • Wakati wa kifo cha Mzee Ibrahimu  watoto wake wote walishirikana katika huduma ya mazishi;Ibrahim akafariki, naye akafa katika uzee mwema . . . Isaka na  Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni bin Sohari Mhiti,lielekealo Mamre .”(Mwanzo 25:8-9); Kwa wakati wetu kinachoshangaza kutokana na misimamo yetu ya Imani tofauti zinazopishana vitabu vya Mwenyezi Mungu tumediriki hata kutoshirikiana katika mambo ya msingi kama majanga ya Misiba njaa na magonjwa; hebu tufuate vitabu tuendeleze umoja wetu kati ya wakristo na waislamu tusimamishe Itikadi ya vitabu.Wakati Nabii Musa alipomuua Mmisri alikimbilia kwa Yethro mtoto wa Midiani na mjukuu wa Ibrahim kwa Ketura mke wake wa tatu;na akatunzwa huko na hawa Waarabu weusi mpaka Mzee Yethro alipompatia Sipora binti yake awe mkewe. (Kutoka 2:15 ;Mwanzo 25:1 – 2);Neno la Mungu linatupatia majina ya huu uzao wa Ibrahimu kwa Ketura kwa kusema Na wana wa Ketura,suria yake Ibrahimu; yeye  Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani na Ishbaki na Shua.Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani.Na wana wa Midiani;Efa, na Eferi na Hanoki, na Abida na Eldaa.Hao wote ndio wana wa Ketura(1Nyak.1:32-33); watoto hawa wa Ketura ni mababu wa zamani wa makabila mengi ya Kiarabu.( Keturah-American Tract Society Dictionary)
  • Wakati Yesu(Masihi Isa) alipozaliwa tunaona Waislamu(Mamajusi wa mashariki) walikuja mpaka Bethlehemu ya Uyahudi wakiifuata nyota  yake  mashariki wakamsujudia na kumpatia dhahabu,Uvumba na manemane. ( (Mathayo 2:8- 11) Hawa walikuwa Waarabu (waislamu) ;Tunaona wachungaji wa kondoo Waebrania nao wanapewa ujumbe wa kuzaliwa kwa Yesu (Masihi Isa) na Mungu alitumia kundi la malaika kuwajulisha habari hiyo ya pekee(Luka 2:8-13). Mwenyezi Mungu alijua kuwa Waarabu(Waislamu) na Waebrania(Wakristo) ni watoto wake kupitia kwa baba mmoja kwa uzazi ila wenye tamaduni tofauti naye akapitia katika tamaduni hizo kuwajulisha habari hii kubwa ya kuzaliwa kwa Masihi Isa(Yesu); Kwa Waarabu Mamajusi alitumia  ndoto na nyota ya mashariki kuwaonyesha Yesu alikozaliwa ila kwa Waebrania alitumia kauli ya malaika; kwani ilikuwa ni muhimu kwa watu wote kujulishwa kuzaliwa kwake kwa sababu siku ya kyama(yawm qyamat) atakayehukumu ni   Masih Isa(Yesu) au mfalme wa Wafalme kwa kiarabu ni Malik-al-Amlak.(Al-Bhukhari Vol.8, Hadith 224,uk.16)
  • Mtume Muhammad SAW akiwasisitiza Waislamu kufuata mafundisho ya wayahudi na Wakristo Inchi kwa Inchi Abu Said Al Khudri amearifu kuwa mjumbe wa Allah (Amani  iwe juu yake) alisema hivi Mwaweza kukanyaga katika njia ile ile ya mapito yaliyopitwa na hao inchi kwa inchi na hatua kwa hatua hasa,ili kwamba kama watatumbukia kwenye shimo lenye mjusi(guruguru), nanyi mfuatane nao humo pia.Tukasema:Mjumbe wa Allah,unamaanisha Wayahudi na Wakristo(Kwa maneno yako) wale wa kabila yenu? Akasema: Sasa ni nani mwingine zaidi ya makundi hayo ya dini? (Sahih Muslim Vol.8 Hadith # 6448 uk.39- Following the Footsteps of the Jews and the Christians)
  • Mwisho kabisa tunaona hata swahaba wa Mtume Muhammad akitumia jengo la kanisa kuswalia kama inavyosimuliwa na Umar Said akisemaHatuingii katika kanisa lenu sababu ya Sanamu na picha,Ibin Abbas amekuwa akiswali ndani ya kanisa  alilopatiwa  kwa sababu hapakuwa na sanamu ndani yake(Sahih Al Bukhari Vol.1,Hadith # 54 uk.254,The book of Salat,To pray in a Church,or in a Temple etc)
Leo hii, tumegawanyika tumegombana, ila ni kwa sababu ya Ibilisi la sivyo tungeendelea na umoja wetu. Maana sote tunatoka kwa Baba mmoja ambapo Imani zetu zimejengeka. Naam ndiye Ibrahim na ndiyo maana hata Mtume Muhammad na Maswahaba wake walitambua umoja huu wa muhimu;Mwenyezi Mungu ametoa ahadi ya agano kwa Waislamu na wakristo akijua kuwa wote ni watoto wa baba mmoja ambao ni wake na siku moja tutarejea. (Inalillah … Wa Inalillah rajun). Na ndipo anatuasa kwa kusema maneno haya katika Torati kitabu cha kwanza Nabii Musa akisema Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe……. Kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako . . . .”( Mwanzo: 17:7 – 8). Kwa hiyo ndugu msomaji hapa tumegundua kuwa wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja Ibrahimu Wakristo ni uzao Isaka na Waislamu Ishmail hivyo ni vema tutambuane na kuizindua njia ambayo babu yetu Ibrahimu alipitia kwa kumfuata na kumtii Mwenyezi Mungu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni