Ifuatayo ni mikao nane ambayo inakubalika katika maombi
i. UKIWA KIFUDIFUDI (PROSTRATE): “Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya
sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani
mwao.”Joshua 7:6;
ii.
UKIWA UNATEMBEA (WALKING): “Kisha akarudi akatembea nyumbani
huko na huko mara moja; akapanda akajinyosha juu yake; mwili wake yule mtoto ukaanza
kupata moto”2Wafalme 4:35
iii.
UKIWA
UMESIMAMA (STANDING): “Ndipo
wakasimama madarajani pa Walawi . . .
wakamlilia Bwana, Mungu wao, kwa sauti kuu.”Nehemia 9:5; “Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni ,mkiwa na neno juu ya
mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe,
ninyi makosa yenu.” Marko 11:25;
“ Yule Farisayo akasimama akiomba
. . . Lakini yule mtoza ushuru alisimama
mbali wala hakudhubutu hata kuinua
macho yake mbinguni bali alijipiga-piga kifua akisema , Ee Mungu, uniwie radhi
mimi mwenye dhambi .” Luka 18:11,13
iv.
UKIWA UMEINUA MIKONO JUU (WITH UPLIFTED HANDS): “Akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA,
machoni pa makutano wote wa Israeli, akanyosha mikono; maana Suleimani alikuwa
amefanya mimbari ya shaba . . . na
kusimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano
wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni.” 2Nyakati 6:12-13; “Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa
jina lako nitaiinua mikono yangu.” Zaburi
63:4;
v.
UKIWA UMEKAA (SITTING): “Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za Bwana; akasema,
Mimi ni nani , Ee Bwana Mungu, na nyumba
yangu ni nini , hata umenileta hapa? . . . kwa maana wewe umemjua mtumwa
wako . . . Ee Bwana hakuna mwingine kama
wewe wala hakuna Mungu mwingine ila wewe . . .” 1Nyakati 17:16-20
vi.
UKIWA UMEPIGA MAGOTI (KNEELING): “Hata ikawa, Suleimani alipokwisha
kumwomba Bwana maombi hayo, na dua hiyo yote ,akasimama na kuondoka hapo mbele
ya madhabahu ya Bwana, hapo alipokuwa amepiga magoti, na kuikunjua
mikono yake kuelekea mbinguni.”1Wafalme 8:54; “”Mwenyewe akajitenga nao
kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba”Luka 22:41; “Petro akawatoa
nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti . . .
.” Matendo 9:40
vii.
UKIWA UMESUJUDU (BOWING): “Musa akafanya haraka akainamisha kichwa chake hata nchi
akasujudu” Kutoka 34:8;
“Ezra akamhimidi Bwana, Mungu Mkuu . Nao
watu wote wakaitikia, Amina, Amina, pamoja
na kuinua mikono yao ; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu Bwana
. . . .” Nehemia 8:6; “Naam, Wafalme
wote na wamsujudie ;Na mataifa yote wamtumikie”Zaburi 72:11
viii.
UKIWA
UMELALA MACHO (SLEEPING): “Basi Hezekia
akajigeuza , akaelekeza uso wake ukutani
, akamwomba Bwana . . . .”2Wafalme
20: 2
Katika
mikao yote hakuna ambao ni bora zaidi ya
mwingine ila cha muhimu sana ni ile nia ya mwombaji au roho ya maombi ya dhati
hivyo waweza ukaomba ukiwa mahali popote na kwa mkao wowote. Mwandishi Ellen G.
White anakubaliana na kauli hii kwa kusema kuwa “Hakuna wakati
wala mahali pasipofaa kumwomba Mungu. Hakuna kinachoweza kutuzuia tusimwinulie
mioyo yetu tukiwa na roho ya maombi ya dhati. Tukiwa katika makundi ya watu
mitaani, katikati ya shughuli zetu za kazi, tunaweza kupeleka dua zetu kwa
Mungu, na kumwomba atupe uongozi wake, kama alivyoifanya Nehemia alipotoa ombi
lake mbele ya Mfalme Artashasta. Chumba cha siri cha mawasiliano kinaweza
kupatikana po pote tulipo. Mlango wa moyo
wetu ungefunguliwa wazi daima, na mwaliko wetu ungepanda juu ili Yesu aje na
kukaa ndani ya moyo wetu kama mgeni atokaye mbinguni.”[1]
ix.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni