SOKA IGIN

WE INSPIRE AND EMPOWER FOR CHRIST'S MISSION.

Jumatatu, 19 Machi 2018

SABABU ZA UMASIKINI


Umaskini,Ni upungufu w kipato cha kuweza kutosheleza mahitaji ya muhimu,Lakini pia umasikini humaanisha upungufu wa mahitaji ya lazima kwa binadamu kama vile upungufu wa chakula kwa jamii,ukosefu wa maji,ukosefu wa matibabu,malazi bora,pamoja na kutojua kusoma na kuandika(Daily news march 14),Maana nyingine ya umasikini ni hali ya kukosa chakula na fedha(Collins English Dictionary).Hizi ni baadhi tu ya maana za umasikini.
SABABU KUMI NA MBILI ZA UMASIKINI

Kukosa uaminifu kwa MUNGU, "Fedha ni mali yangu,na dhabihu ni mali yangu,asema Bwana wa majeshi." Hagai 2:8,Kila kitu kilicho chini ya jua ni mali ya MUNGU,Hivyo ni muhimu sana kuwa waamiifu kwa MUNGU, na kwa wanadamu wenzetu ambao ni watoto wa MUNGU.Lakini pia ukumbuke kua kuna vitakatifu vya MUNGU ambavyo vikiguswa tu Mungu mwenyewe huingilia kati kutetea utakatifu wake,vitu hivyo ni Zaka na sadaka,Tunaposhindwa kuwa waaminifu wa kurudisha zaka na sadaka Mungu huondoa mibaraka yake kwetu.Haipaswi kugusa zaka na sadaka ya MUNGU Maana ni takatifu.Mungu ameahidi laana kwa wale watakao gusa.

Kukosa elimu,"Ewe mvivu,mwendee chungu,zitafakari njia zake ukapate hekima.kwa maana yeye hana akida wala msimamizi ,wala mkuu,lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua;hukusanya chakula chake wakati wa mavuno"Mithali 6:6-8.
MUNGU ametoa namna mbalimbali za kupata elimu.kuna elimu ambayo unazaliwa na kufundishwa kwa kuona na kusikia,lakini pia MUNGU akaweka watu,wanyama na mimea ili tuweze kujifunza(Informal education) na elimu nyingine ni elimu ya darasani ambazo baadhi yetu tumefanikiwa kuzipata(formal education) Wengi wetu tumekua masikini kwa sababu ya kuzipuuza elimu hizi,na wengine tumesoma elimu za darasani tukafaulu lakini hatukuelimika yaani hatuja thubutu kuzitumia katika vitendo.Hii imesababisha umasikini wetu.

Kukosa mipango au kukosa kujiwekea malengo na kuyafikia katika maisha,Mipango au malengo ni uelekeo ama dira,Kushindwa kuwa na mipango na malengo kunatufanya kushindwa kufika tunakokwenda,Zifuatazo ni kauli na majibu ya watu ambao hawana mipango wala malengo ya kufikia katika maisha,SWALI:Unategemea kwenda kusomea nini baada ya mtihani wako wa kidato cha sita? JIBU: Nasubili wanipangie  wenyewe huko kwenye baraza la mtihani.SWALI:Unataka kuolewa na mwanaume wa namna gani? JIBU: Yeyote atakaye tangaza nia ya kunioa.Ndugu msomaji je majibu yako yangekuaje kama ungeulizwa maswali haya,kumbuka kuwa haya ni majibu ya watu ambao hawana malengo ya kuyafikia katika maisha na hii ni sababu kubwa ya umasikini.

Familia za pembeni yaani mlundikano wa ndugu nyumbani bila kufanya kazi yeyote bali kula na kulala tu."Ndugu twaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo,jitengeni na nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu,wala si kwa kufuata  mapokeo mliyoyapokea kwetu.mwajua wenyewe njinsi iwapasavyokufuata;kwasababu hatukuenda bila utaratibu kwenu ;wala hatukula chakula kwa mtu yeyote bure;bali kwa taabu na masumbufu,usiku na mchana tulitenda kazi,ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote" 2Wathesolanike 3:6-8 Neno la Mungu linakataza tabia ya kukaa na kuzurura kivivu na hata jamii  haifurahii tabia hiyo!.Tabia hii inachangia umaskini kwa kiasi kikubwa haswa pale mtafutaji mmoja katika familia moja ndiye anayetegemewa kulisha,kuvisha na kutibu watu zaidi ya wanane waliokaa nyumbani kwake ambao siyo wazee wala wagonjwa ambao kazi yao ni kula,kuoga,kukaa sebuleni na kutazama TV masaa yote na kwenda kulala.

Afya mbaya,"Lakini itakua usipotaka kusikiliza sauti ya Bwana Mungu wako,na usiyaangalie kuyafanya maaagizo yake yote na amri zake,nikuagizayo hivi leo ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata...Bwna atakupiga kwa kifua kikuu,na kwa homa na kwa kuwashwa,na kwa hali ya moto na kwa upanga na kwa ukaufu na kwa koga;navyo vitakufukuza hata uangamie."(Kumbu28:15-22) Kimsingi hakuna anayetuma maombi ili apate ugonjwa maandiko yanathibitisha kuwa chanzo cha magonjwa mengi ni kukosa uaminifu kwa Mungu yaani kuto msikiliza Mungu.Magonjwa yamekua chanzo cha umasikini  kutokana na kuongezeka kwa gharama za maisha watu wanaomuguza mgonjwa inawagharimu kujipanga kwa usafiri,dawa chakula n.k.Mara nyingi familia zinazouguliwa  imekua vigumu kuendelea kiuchumi badala yake wameangukia katika wimbi la umasikini mkubwa hasa pale walipomtibu mginjwa kwa muda mrefu.

Uvivu,ulegevu na utepetevu,"Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi;hivyo wakati wa mavuno ataomba hana kitu" (Mithali 20:4)Kwakifupi waweza kusema kuwa mvivu ni ombaomba,anaousingizi mzito wa kiakili na kimwili,ni mjuaji ana hekima machoni pake mwenyewe na chakutisha hawa wavivu ni ndugu  wamoja na shetani/mharabu;mwandishi mmoja wa mambo ya kiroho anasema"Mawazo yasiyotumikishwa ni karakana ya shetani".sababu kubwa ya umasikini ni Uvivu,ulegevu na utepetevu.

Akili gonjwa/iliyougua kwa na kulemaa kwaajili ya misaada"Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa" (Mithali 13:4)Mtu aliye na akili gonjwa(mvivu) au aliye lemaa kwaajili ya misaada,yeye hata ukimpatia biashara au mradi wa kumwingizia  kipato hataweza kuuendeleza kwani akili yake bado ni changa sana kwenye upande wa kujitegemea.na hiki ndicho kinachowafanya watu wengi kupanga utaratibu wao wa maisha wakitegemea fedha za ndugu zao,marafiki zao, wazazi wao n.k. watu kama hawa mazungumzo yako maneo kama mfadhili,kuwezeshwa,kupigwa tafu,kusaidiwa na kubebwa siyohaba katika midomo yao watu kama hawa hulaumu serikali kuwa haijawawezesha,Baba hajanisomesha mpaka chuo kikuu,mume wangu hajaniwezesha kimtaji n.k

Ukosefu wa ardhi,Mungu alijua kuwa ardhi ni muhimu kwa mafanikioya taifa lake la Israeli na ndiyo maana alipokua anawaandaa kuingia nchi ya kaanani alimwambia Yoshua kuwa,kila mahali zitakapo kanyaga nyayo zenu ,nimewapa ninyi,kama nilivyomwapia Musa(Yoshua 1:3-4).Hivyo basi kukosa Ardhi ni sababu kubwa sana ya umasikini.lakini kwa nchi kama Tanzania shida hiyo hakuna labda mtu mwenyewe kwa utashiwake aamue kuikimbia ardhi kama wengine tunavyohama kutoka vijijini na kukimbilia mjini ambako hakuna ardhi ya kutosha."Alimaye shamba lake atakua na chakula tele;bali afuataye mambo ya upuuzi hana ufahamu".(Mithali 12:11).

Kuridhika kuishi maisha duni,Baadhi ya watu wana hali ya kuridhika kuishi maisha duni na hii inasababishwa na hali ya kutokutaka kujifunza na kukabili changamoto za maisha.Kulidhika kuishi maisha duni hali hii inachangiwa hasa na kuwa na mawazo hasi ya masiha kwa baadhi ya watu hasa haswa kuhusu kujitegemea wakiwa wamevisha joho zuri la dini ikiwa ni pamoja na kuitafuta mistari ya biblia ambayo wanadhani inaendana na mitazamo hiyo ya kuishi maisha duni kama mistari hiyo ingesomwa kwa maana halisia haimanishi mawazo hayo.

Kiujumla,kabla ya dhambi kuingia katika sayari yetu,Umasikini haukuwepo.umasikini ni mojawapo ya matokeo ya dhambi baada ya mwanadamu kuingia dhambini.Mungu ameahidi kutufaya vichwa na siyo mkia pale tutakaposikiliza maagizo yake(Torati 28:13).Mungu ameahidi kuwa hatutakuwa masikini kama tutadumu kuwa waaminifu kwa maagizo yake"Lakini hakutakuwepo maskini kwenu;kwakua Bwana atakubarikia kweli katika nchiakupayo Bwana Mungu wako,uimiliki,iwe ulithiwako".(Kumb 15:4)

Mada hii imatolewa katika kitabu cha "Dawa ya ugonjwa wa umasikini imepatikana" Mwandishi IGIN JOHN SOKA.Ukrasa wa 11,14-22. Mada zingine katika kitabu hiki ni, SAYANSI YA BIASHARA,JINSI YA KUBUNI BIASHARA,UFUGAJI WA KUKU CHOTARA,KILIMO CHA PESHENI,KAMA MNAATAKA MALI.
KITABU HIKI KIMEKUA MSAADA MKUBWA KWA WATU.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni