FAIDA SITA (6) ZA KUFANYA KAZI.
.
Zifuatazo ni faida za kufanya
kazi..
1. Kazi husaidia mwili kuwa na afya njema.
“BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.” Mwanzo 2:15;
Wazazi wetu walikuwa hawana shida ya njaa wala chakula kwani walikuwa na chakula tele. Ilikuwa ni mpango wa Mungu mwanadamu afanye kazi kwa faida ya mwili wake na kukuza akili yake
- Kazi zinarefusha maisha.
Ukitaka mtu afe mapema mweke
tu ale na kwenda haja bila kushika kazi yoyote, hatima yake ni kaburi
- Kazi inaleta mabadiliko katika mapafu na mzunguko wa damu inayowezesha vitu hivyo kufanya kazi vizuri na kupunguza sonona/ huzuni na ‘simanzi.’
- Kazi inawezesha msukumo wa damu kuwa wa kawaida.
- Mapigo ya moyo na Msukumo wa damu hurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi.
- Mishipa ya moyo inakomazwa pale tunapofanya kazi.
- Kazi inaboresha afya ya moyo na kudhibiti magonjwa ya moyo, pamoja na kupunguza ukali wa shinikizo la damu na kuharakisha kupona kwa mwili.
- Kazi inaongeza uwezo wa moyo kusukuma damu.
- Kazi inapunguza mafuta ndani ya damu .
- Inasaidia kulala na kupumzika vizuri pamoja na kuondoa harara
- Kazi inaboresha uwezo wa kuyeyusha chakula, kwa kuongeza mtikisiko wa tumbo unaosaidia chakula kuyeyuka na kunyonywa vizuri mwilini.
- Kazi za mikono huchelewesha uzee.
- Kazi husaidia misuli kuwa na hali nzuri na kuboresha uzuri wa mwonekano pamoja na uwezo kuvumilia
2. Kazi Huleta Heshima.
“Je wamwona mtu mwenye bidii katika kazi
zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.” Mithali
22:29
Kumbuka Mtu mzembe hata mkutano wa ubalozi
wa nyumba kumi kumi hawezi
kukaribishwa; hata hawezi
kupewa kadi ya mchango
wa harusi. Mtu anatambulika kwa kazi yake
3. Kazi huleta Shibe Nyumbani.
“Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo
ya upuuzi atapata umaskini wa kumtosha.
(Mithali 28:19).
Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; hivyo wakati
wa mavuno ataomba, hana kitu. Mungu
hatatuma malaika kumlimia mtu shamba,
hata mtu aombe na kufunga mwaka mzima bila kufanya kazi huyo hatavuna kitu. Chunguza lishe ya mtu au familia isiyokuwa na mpango maalum wa kazi au yenye muda mwingi wa kupumzika. Chakula cha mtu au familia kama hii ni cha shida na kisichokidhi matakwa ya lishe mwilini. Mithali 20:4
4. Kazi Huondoa Umaskini.
“Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo
ya upuuzi atapata umaskini
wa kumtosha.Mithali 28:19.
Siri kubwa ya kuondokana na umaskini ni kumwamini Mungu kufanya kazi kwa bidii.
5. Kazi Huondoa Fedheha
"Maskini huchukiwa hata na jirani yake; bali tajiri ana marafiki wengi"Methali 14:20 ; Ukitaka kuepuka fedheha fanya kazi kwa bidii utafanikiwa tu. Ahadi za Mungu ni za kweli
kama Daudi asemavyo kuwa ”Nalikuwa
kijana nami sasa ni Mzee sijamwona mwenye haki ameachwa wala uzao wake akiomba
chakula” Zaburi 37:25.
6. Huondoa Ukoloni mambo leo.
"Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye"Methali 22:7. Kuna ukweli mkubwa katika usemi huu wa Sulemani mwenye hekima.
Mtu asipotaka kufanya kazi, atatawaliwa na tajiri anayemkopesha na
kumwajiri. Mtu anayejitegemea analinda utu wake
daima.
KWA MAFUNDISHO ZAIDI YA UJASIRIAMALI JIPATIE SETI YA VITABU VIWILI
1. Dawa ya Ugonjwa wa Umaskini imepatikana@10,000
2. Mjasiriamali na Ujasiriamali @10,000
Mawasiliano na Mwandishi : Telephone contacts: 0788010398 au 0755393278
:E-Mail contacts: sokaigin@gmail.com au sokai@aua.ac.ke

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni